The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya SADC


Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Agosti, 2019.


 

Mhe. Rais, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuwezeshe ili uongozi wako kwa kipindi husika uwe wa kutukuka katika kuendeleza maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ndani ya nchi Wanachama wa SADC.


 

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki SADC, Mungu ibariki Tanzania.2019-08-19 11:10:40Rais wa Tanzania na Afrika Kusini kwa pamoja wameshiriki Kongamano la biashara na uwekezaji, Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa wameshiriki kama Wageni Rasmi kwenye kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Kongamano hilo limefanyika tarehe 15 Agosti, 2019 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam sambamba na Mkutano wa Wakuu wa Nchini wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)


Katika hotuba yake, Mhe Dkt. Magufuli amesema kwamba Afrika Kusini imepiga hatua katika maendeleo, technolojia na mitaji. Hivyo amewakaribisha kuja kuwekeza Tanzania kwenye kuongeza thamani madini, mazao ya kilimo (pamba), uvuvi, ufugaji (nyama na ngozi), uzalishaji wa mafuta ya kula, sukari, uunganishaji wa magari, uzalishaji wa madawa na vifaa tiba. Lengo ni kuiwezesha nchi kufikia hatua....

2019-08-16 18:30:15Kampuni ya Ambiance Distilleries (T) Ltd kuendelea na uzalishaji wa vinywaji vikali 'spirit' huko Bukoba.


Agosti, 2019: Kampuni ya Ambiance Distilleries (T) Ltd imesajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuendesha mradi wa kuzalisha vinywaji vikali 'spirit' huko Bukoba. Mradi unamilikiwa kwa ubia kati ya Mtanzania na Mganda na ulipewa cheti cha Uwekezaji June, 2018 na kuanza uzalishaji Januari, 2019

 

Wakati uzalishaji unaendelea kulijitokeza changamoto ya kutoelewana kati ya TRA na kampuni hiyo kuhusu masuala ya kodi ambapo ilifikia hatua kampuni kusimamisha uzalishaji. Mwekezaji alifikisha taarifa hizo TIC na baada ya Kituo kupokea taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe ameamua kufika Bukoba na kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Marco Gaguti kisha kufanya mazungumzo na pande zote mbili kwa kuondoa/ kutatua changoto husika sambamba na kurejeza kiwanda katika uzalishaji.

 

Baada ya mazungumzo, TRA na kampuni ya Ambiance wameafikiana na....

2019-08-07 13:12:30Utatuzi wa changamoto za wawekezaji nchini huchochea zaidi uwekezaji. Ubalozi wa Uingereza waahidi kuunga mkono jitihada hizo.


 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe leo tarehe 29 Julai,2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke. Miongoni mwa mambo ambayo Mhe. Balozi amezungumzia ni kwamba wanafurahishwa na hatua mahsusi zinazochukuliwa na Serikali katika kutatua changamoto za wawekezaji. Jambo hilo ni muhimu kwa kuwa linawapa wawekezaji imani na kuwahamasisha zaidi kuwekeza.

 

Mhe. Cooke ‘natoa pongezi kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa niaba ya Serikali kwa hataua mnayochukua kila mara katika kutatua changamoto mbalimbali za uwekezaji ambazo sasa zinazaa matunda na zinashawishi uwekezaji. Tutaendelea kuunga mkono jitihada hizo’

 

Katika kufanikisha zaidi, Mhe. Cooke amesema ni vema kuendelea kuwapo kwa jitihada mahsusi za mashirikiano zaidi kati ya TIC na Ubalozi wa Uingereza ili kushauriana na kusaidia mikakati yenye lengo la kuboresha....

2019-07-29 16:06:36anzania Investment Centre (TIC) which is the first point of call for investors in Tanzania welcomes to Tanzania the 39th SADC Summit participants


Dear SADC Delegates,

It is a great honour to us as a nation to host the Summit of Heads of State and Government of the Southern African Development Community (SADC) from 5th -18th August, 2019.

 

Tanzania Investment Centre (TIC) which is the first point of call for investors in Tanzania welcomes to Tanzania the 39th SADC Summit participants from different nations. Please, enjoy your stay while thinking about investing in Tanzania, the country endowed with abundant investment opportunities.

 

You may choose to invest in various sectors such as Agriculture, Manufacturing, Tourism, Edible oil, Infrastructure network, Cane sugar production, Pharmaceutical and Medical equipment, Cotton and Textile, Livestock and Leather Industry, Fishing and Aquaculture, Mining and Metals.

 

Investors wishing to invest in the country will be facilitated through TIC....

2019-07-29 15:55:05
Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)