The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTREKongamano la Kwanza la Kimataifa la Kibiashara 'Tanganyika Business Summit & Festival’ litafanyika Mkoani Kigoma tarehe 9 - 11 Mei, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa NSSF. .


Ndugu Wadau wa Biashara na Uwekezaji nchini;

 

Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Local Investment Climate (LIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Baraza la Biashara Tanzania (TNBC), Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA),Kigoma Joint Programm(KJP),International Trade Centre (ITC) na Afro Premiere kwa pamoja wanaandaa 'Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kibiashara' maarufu kama 'Tanganyika Business Summit & Festival’. Kongamano hilo la aina yake litafanyika kwa siku tatu Mkoani Kigoma kuanzia tarehe 9 mpaka tarehe 11 Mei, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa NSSF. Mgeni rasmi atakuwa ni Mhe.Samia S. Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Pamoja na mambo mengine, kongamano lina lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla na wafanyabiashara wa nchi jirani za Burundi, DRC Kongo, Zambia, na Rwanda ili kwa pamoja kujadili na kuafiki namna ya kukuza biashara na uwekezaji kutokana na fursa zilizopo ndani ya nchi hizi hususan kwenye sekta lengwa pamoja na kuibua fursa mpya.

 

Sekta zilizolengwa ni viwanda, kilimo na uongezaji thamani; mifugo na uongezaji thamani, uvuvi na uongezaji thamani, usafirishaji; uongezaji thamani chumvi na ufungashaji na biashara kwa ujumla.

Kongamano linatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 300 na litaambatana na maonesho (Exhibition) ya bidhaa na huduma mbalimbali kutoka Tanzania, Burundi; DRC Kongo, Rwanda na Zambia ambapo pia zaidi ya waoneshaji 150 watashiriki.

 

Watanzania kutoka Mikoa yote mnaalikwa kuchangamkia fursa hii kwa kushiriki kongamano ili kunufaika na fursa mbalimbali zitakazojitokeza ikiwa ni pamoja na kunadi fursa za biashara na uwekezaji, kujifunza mbinu mpya za biashara na uwekezaji kutoka kwa washiriki sambamba na kutafuta wabia, masoko, mitaji na teknolojia.

 

Kwa maelezo zaidi ikiwamo usajili, tafadhali piga namba za simu namba +255 745875774 au 255 756528022 au +255 754750076

Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)